Tumgik
#kadiria gharama ya ujenzi
hamiahapa · 3 years
Text
JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO - S1
SEHEMU YA KWANZA: MAHESABU YA IDADI YA TOFALI ZINAZO HITAJIKA KWAAJILI YA UJENZI WA MSINGI NA KUTA (TOFALI ZA BLOCK)
Habari wana Ujenzi!, nimegundua watu wengi wanapata changamoto ya kufahamu makadilio ya material wanayo hitaji katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali. Kwasababu hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo tutaanza na mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga.
youtube
Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo
1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako. Ramani inachorwa na wasanifu majengo wataalamu ambao wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu katika vyuo vinne tu hapa nchi navyo ni Ardhi University (chuo kikuu), na vyuo vya kati Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute — Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam.
2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni hydraform, tofali za kuchoma ama blocks, hii ni kwasababu tofali zina tofautiana size ama ukubwa hivyo hata idadi yake itakuwa tofauti. Tofali zipo za aina tatu, ukubwa wake ni (length x width x thickness/urefu x upana x unene)
HYDRAFORM; 90 mm x 240 mm x 40 mm
BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm
KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm
Tumblr media
Hapa tuta tumia mfano wa nyumba hii yenye vyumba viwili-kimoja kikiwa na choo/bafu ndani, sebule, jiko, choo cha wageni na vibaraza viwili; kufanya mahesabu ya tofali zetu.
Hapa kuna hatua mbili za kufuata
1. Tafuta eneo la kuta zote
2. Jumla ya eneo lote la kuta gawanya kwa ukubwa wa tofali
KUTAFUTA ENEO LA KUTA
Hapa tuta tumia kanuni ifuatayo
Eneo = Urefu( wa kuta) x kimo (urefu wa ukuta kwenda juu)
Sasa kujua urefu wa kuta zote, utatakiwa kujumlisha urefu wa kuta zote
Kwenye mchoro wetu pale juu nime weka namba kila kuta hivyo itakuwa kama ifuatavyo {vipimo vipo katika milimita (mm)}.
1 m = 100 cm = 1,000 mm; 1 cm = 10 mm
Ukuta 1= 6,500 mm; ukuta 2 = 9,150 mm; ukuta 3 = 4,000 mm; ukuta 4 = 4,000 mm; ukuta 5 = 9,450 mm
Ukuta 6=11,046 mm, ukuta 7=6196 mm +3200 mm, ukuta 8=9,101 mm, ukuta 9 =3,060 mm, ukuta 10 = 2,900 mm
Sasa uki jumlisha kuta hizo zote unapata jumla ya = 68,603 mm
Eneo la kuta = urefu wa kuta x kimo cha kuta
Hapa kama utajenga nyumba ya kozi 13 maana yake ni kimo cha 3000 mm
Hivyo eneo litakuwa = 68,603 x 3000= 205,809,000 mm
Sasa kumbuka tuna sehemu za wazi ambazo hizi hazihitaji tofali, mfano milango, madirisha na sehemu za wazi za vibaraza
Kanuni ni ile ile urefu x kimo:
Tuna madirisha 6 yenye urefu 2,000 mm & kimo 1,800 mm= 2000 x 1800 sawa na 3,600,000 mm
sasa, tuna madirisha sita yenye vipimo sawa hivyo 3,600,000 x 6 = 21,600,000
Tumia dirisha 1 lenye urefu 1,400 na kimo 1,500 = 1,400 x 1500 sawa na 2,100,000 mm
Tuna dirisha 1 lenye urefu 1,000 na kimo 1,800 = 1,000x1, 800 sawa na 1,800,000 mm
Tuna madirisha 2 yenye urefu wa 800 na kimo 600 = 800x600 sawa na 480,000 mm
480,000 zidisha kwa 2 sawa na 960,000 mm
Tuna milango 9 yenye urefu wa 900 na kimo 2,400 = 900 x 2,400 sawa na 2,160,000 mm
2,160,000 zidisha kwa 9 sawa na 19,440,000 mm
Uwazi wa vibaraza jumla uref 10,010 kimo 2,400 =10,010 x 2,400 sawa na 24,024,000 mm
Jumla ya wazi = 21,600,000 + 2,100,000 + 1,800,000 + 960,000 +19,440,000 + 24,024,000 = 69,924,000 mm
Eneo kamili linalo hitaji tofali za kuta lita kuwa
ENEO LA KUTA — ENEO LA WAZI0 = 205,809,000–69,924,000= 135,885,000 mm
hivyo basi, IDADI YA TOFALI, itakuwa kama ifuatavyo:
Sasa urefu wa msingi wako utategemea na nature ya eneo lakini tuchukulie utakuwa na urefu wa 900 mm, ambapo ni sehemu tambarare (isiyo korofi)
Kumbuka jumla ya urefu wa kuta zote ni 68,603 mm
Kwahiyo 68,603x900 = 61,742,700 mm
Kwahiyo kupata tofali tutalazimika kuchukua jumla ya ukubwa wa kuta ukiwa umetoa uwazi na jumla ya eneo la kuta za msingi kisha tuta gawanya kwa eneo la tofali moja
135,885,000+61,742,700= 197,627,700 mm
Kumbuka tofali ya block lina urefu wa 450 mm na kimo cha 230 mm
Hivyo eneo la tofali ni 450 x 230=103,500 mm
Idadi ya tofali itapatikana kwa 197,627,700mm/103,500mm = 1,909 matofali
Hapa utahitaji kuongeza asilimia kidogo ya tofali kwaajili ya zile zitakazo vunjika na ngazi pia, tutatumia 5%, kwahiyo jumla ni tafali 1909+ 0.05(1909) = 2,004.45 ≈ 2,000 tofali
MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA YAKO
hapa tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako.
NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe sawa kwa asilimia 100, lakini mara nyingi yanakaribia ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana
Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000
Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS
Hapa tuseme idadi ya tofali za Msingi (inch 6) ni tofali 700
Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1300
A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI ZA INCH 6)
-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa
-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga Zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)
KANUNI
Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6- za kulaza)
Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo
Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement
NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza). Hii hufanywa ili kupunguza gharama japo kama ni kwenye kiwanja korofi inaweza kuleta shida.
B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)
-Tofali hizi mara nyingi hujengwa kwa kusimama hivyo hazili mchanga na cement nyingi kama zile za msingi
KANUNI
Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)
Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo
Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement
NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama), pia hii ni ili kupunguza gharama.
NB: KIPIMO CHA MCHANGA
Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA
Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA
Tumblr media
Katika makala ijayo tutaendelea na kujumlisha gharama za usafirishaji, gharama za malighafi ya kumalizia nyumba (finishing) na nyinginezo.
Tunatoa ushauri wa kitaalam na kufanya ujenzi, usanifu majengo (ramani) & kukadiria gharama za ujenzi. Tafadhali tuandikie maoni (comment) yako hapo chini & kisha washirikishe (share) na wengine makala hii.
9 notes · View notes