Tumgir
#AMFisH
imungy-blog · a year ago
Text
Tumblr media
Bwana mmoja alilima shamba katika Jangwa, Basi nyani wakaonelea kula mazao kwa Bwana yule kwa kila mwaka alipopata kulima. Bwana yule alipata hasira sana na ikawa anawafukuza wale nyani kila mara anapowaona shambani.
Jitihada yake yote ya kufukuza nyani haikuwafanya nyani wakose moja kwa moja kuiba mazao katika shamba la bwana yule. Siku moja nyani wakaitisha kikao ili wajadiri hadha na usumbufu unaowapata kutokana na Bwana yule hasa wanapotaka kupata chakula.
Nyani waliona wananyanyasika sana na hata kuona huenda Mungu wao kawaacha au ni ule ujinga wao wa kutopeleka malalamiko yao kwa Mungu wao,
Nyani wakakubaliana wamuombe Mungu wao amfishe(ampe mauti)Bwana yule ili wao wapate wasaa mzuri wa kula mazao shambani. Mungu wao akawakubalia na ndani ya wiki moja mkulima akafikwa na mauti akafa.
Nyani walifurahi sana na wakasherehekea kifo cha Bwana mkulima na wakaingia shambani wakijitwika maboga,mahindi, kunde pori na mihogo, Huo ukawa mwaka wa shibe kwa nyani na wakazaliana hata kujaza bonde lilokuwa karibu.
Mwaka uliofuata nyani wakaanza kutembea masafa marefu kutafuta chakula pasipo kufanikiwa, nyani wakaanza kufa hovyo hovyo hali iliyotokana na njaa na ukosefu wa chakula kwa muda mrefu.
Mfalme nyani akaita kikao na kujadili tatizo linalowakabili na hapo ndipo wakabaini ya kwamba kifo cha bwana mkulima ndicho kimepelekea vifo vyao vya njaa kwa kuwa kabla ya bwana mkulima kufa hawakupata vifo vya njaa bali kulikuwa tu na kausumbufu ka kufukuzana hapa na pale.
Ama kweli unaweza kuona mtu fulani kama kikwazo katika maisha yako kumbe ndiye mlinzi wa maisha yako, siku zote usiupuuze mchango wa mtu katika maisha yako Kwani huwezi jua thamani halisi ya mchango wake. #notpolitical #apolitical #hadithi tu.
0 notes
3rdcoastfishin · 2 years ago
Text
@3rdcoastfishin stopping by @seaponybaitandtackle and getting a few things and saw this from @amfishingproducts so I had to get it uv light to make there lures glow.
#3rdCoastFishin #amfishing #seaponybaitandtackle #fishing
Tumblr media
0 notes
tetohina · 2 years ago
Note
guluguluguluguluglugulugulugulgugu
me when i amfish :)
0 notes